KAMATI YA SIASA YA CCM KATA YA NJOMBE MJINI YARIDHISHWA NA UKARABATI UNAOENDELEA JOSEPH MBEYELA
Ziara ya ukaguzi ...huo imefanyika October 5,2026 ikiongozwa na Mwenyekiti wake ndugu Philemoni Simba, Katibu mwenezi wa Chama ndugu Solanus Mhagama, Diwani wa Kata ya Njombe Deo Mawaza walioambatana na watendaji wote wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa pamoja watalaamu mbalimbali na mabalozi.
Mwenyekit Philemoni amesema yeye kama Mwenyekiti chama cha Mapinduzi kinachoongoza Serikali amewapongeza wote waliohusika kubuni wazo hilo na wote waliojitoa kuchangia pesa zao na vifaa kwani hatua hiyo iliyoonekana haikuota kama uyoga bali watu walijitoa mpaka kufikia mafanikio hayo hivyo.
Akisoma taarifa ya fedha Mkuu wa Shule ya Joseph Mbeyela amesema jumla ya ahadi zote zilikua ni zaidi ya Shilingi Milioni Ishirini na Moja na laki Tano (21,500,000/=) lakini pesa iliyokusanywa ni shilingi Milioni kumi na Mbili (12,000,000/=) na ambayo haijakusanywa ni shilingi Milioni Nane(8,000,000/=)
Kiasi kilichobaki mpaka sasa milioni 2 pesa ambayoimetumika mpaka sasa ni Shilingi Milioni Kumi ambapo zimeshuhudiwa grili za milango zimenunuliwa, ujenzi wa uzio na madara vinaendelea.
Akizungumza Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Deo Mazao amemuagiza Mkuu wa Shule ndani ya siku saba waanze kutumia ofisi ya waalimu ambayo imejengwa na kufikia asilimia Tisini kukamilika na awaalike wadau waliochangia pesa zao kwenda kutembelea na kujionea matumizi ya fedha walizochanga.
Lakini pia ameiomba kamati ya Kata iendelee kufuatilia miradi mbalimbali katika kata hiyo kuona nakusukuma kuona inakamilika.
Katibu wa Siasa mafunzi itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi kata ya Njombe Mjini Solanus Mhagama amewapongeza wote amesema jambo hilo lililofanyika ni kubwa na limepokelewa kwa ukubwa na viongozi wa Mkoa na Halmashauri.
Amewapongeza watendaji wote kwa ushirikiano wao akisema ndivyo chama cha mapinduzi kinataka kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano na amesisitiza kwamba endapo jambo litatokea katika kata hiyo basi wao kama chama cha mapinduzi watalibeba kwa ukubwa na kuhakikisha linakamilika na amesisitiza kuwa chama kitasimamia suala la uaminifu.Show More




















