Posted By Bajeti: 2025-01-31 06:42:34 | Last Updated by admin on 2025-04-03 14:53:05
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 62
WASHINGTON DC,MAREKANI
SERIKALI ya Rais mpya wa Marekani Donald Trump imetoa orodha ya wahamiaji wanaotakiwa kuondoka nchini humo huku mpango wa kuwatimua wahamiaji haramu ukianza kushika kasi.
Vyombo vya habari vya nchi mbalimbali ikiwemo Iran vimenukuu taarifa kulingana na stakabadhi kutoka Idara ya Uhamiaji ya Marekani (ICE) ambayo imeweka orodha ya Wakenya 1,282 wameorodheshwa kupakiwa kwenye ndege na kurudishwa nchini mwao wakati wowote kuanzia sasa.
Stakabadhi hizo zinaonyesha idadi kamili ya wahamiaji kutoka kila nchi ambao wanatakiwa kutimuliwa, huku mataifa ya Amerika Kusini yakiwa na idadi kubwa zaidi ya maelfu ya raia.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, mbali na Kenya, imeripotiwa kuwa kuna wahamiaji 393 nchini Marekani raia wa Uganda 301 ambao watatimuliwa huku Tanzania nayo ikitarajiwa kupokea raia wake 301 wanaotarajiwa kurejeshwa nchini humo kutoka Marekani.