Posted By Bajeti: 2025-02-24 02:24:17 |
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 88
NA GOODLUCK HONGO
VIONGOZI wa madhehebu ya dini mbalimbali na waumini wao wanatarajia kushiriki kuliombea Taifa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mbali na kuliombea Taifa na Rais Dkt.Samia lakini pia maombi hayo yatajikita katika kuombea amani na utulivu ikiwemo uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza na maelfu ya waumini wake wa Kanisa la Inuke Uangaze Februari 16,2025 Kawe mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada ya Kesi yako Imekwisha,Mtume Boniface Mwamposa 'Buldoza' amesema ni muhimu kuliombea Taifa hivyo kila mtu anapaswa kushiriki.
Amesema maombi hayo yatafanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam Februari 28,2025 ambapo pia yatahudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa ambavyo vitashiriki katika uchaguzi.
"Siku hiyo chakula mtakula pale pale na tunataka kila mpakwa mafuta atamke baraka juu ya Taifa.
"Ni vizuri kuungana kuliombea Taifa,wote tushiriki kuliombea Taifa na wale wenye magari basi ni muhimu kusaidia kubeba watu"amesema Mwamposa
Akizungumza na malefu ya waumini wake Februari 23,2025 Kawe Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam wakati wa Ibada ya Kula Keki ya Upako,Mtume Mwamposa 'Bulldoza' amesema kutokana na sababu mbalimbali wameamua kufanyia kongamano hilo katika Viwanja vya Leaders Club vilivyo Kinondoni karibu na ubalozi wa Ufaransa.
Amesema kongamano hilo lifanyika kuanzia saa 8:00 mchana badala ya saa 12 asubuni kama ilivyotangazwa awali ili kutoa nafasi pia kwa wafanyakazi kushiriki katika kongamano hilo.
"Mimi mwenyewe Bulldoza nitakuwepo,Rose Muhando atakuwepo na waimbaji wa injili wengine wengi mnaowafahamu"amesema Mtume Mwamposa