Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa

Siasa habari

Posted By Bajeti: 2025-02-01 19:01:57 | Last Updated by admin on 2025-04-02 20:42:02

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 344


Safari ya mafanikio ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na miaka minne ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA  la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa chachu ya mageuzi makubwa katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania, likitimiza jukumu lake la kipekee la kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge Na. 45, Shirika limeendelea kusimamia maono ya waasisi wa Taifa, likiongozwa na Dira ya Maendeleo Endelevu ya makazi.

Hata hivyo, miaka minne ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta kasi mpya na mafanikio makubwa yanayostahili kusimuliwa.

Historia na Maono ya Kuanzishwa kwa NHC

Shirika hili liliundwa kama sehemu ya maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya kuhakikisha mahitaji ya msingi ya mwanadamu yanapatikana kwa urahisi.

Katika miaka ya mwanzo, NHC lilitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za makazi na majengo ya umma, lakini changamoto za kiuchumi na kisheria zilianza kuathiri utendaji wake.

Mageuzi ya kihistoria yalifanyika katika miaka ya 1990 hadi 2008, ambapo sheria zisizokuwa rafiki katika Maendeleo ya Sekta ya Nyumba zilibadilishwa, na NHC likapewa Mamlaka mpya ya kujiendesha kibiashara bila kusahau jukumu lake la msingi.

Hatua hizi ziliweka msingi wa kuboresha huduma za makazi kwa Watanzania, lakini ni katika kipindi cha uongozi wa Dkt. Samia ambapo kasi ya utekelezaji wa miradi ya nyumba imeongezeka kwa kiwango cha kipekee.

Mageuzi na Mpango Mkakati wa Maendeleo

Mwaka 2015, NHC lilianzisha Mpango Mkakati wa Miaka 10 (2015/16 – 2024/25), uliolenga kujenga nyumba 10,000 na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Lakini ni katika kipindi cha Uongozi wa Dkt. Samia ambapo utekelezaji wa mpango huu umechukua sura mpya, ikiwemo uanzishaji wa miradi mikubwa kama “Samia Housing Scheme” ambayo inatarajiwa kuwa zitajengwa nyumba 5,000 katika maeneo mbalimbali nchini.

Mafanikio Makubwa Katika Sekta ya Nyumba na Ujenzi wa Nyumba za Makazi na Biashara

Hadi sasa, NHC limefanikiwa Kujenga zaidi ya nyumba 30,000 za makazi tangu kuanzishwa kwake na linaendelea kujenga nyumba za kuuza na kupangishwa.

Katika kipindi cha Awamu ya Sita, NHC imekamilisha miradi mikubwa ya nyumba za makazi kama vile:Nyumba 887 za makazi katika eneo la  Iyumbu na Chamwino, Dodoma.

Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Chamwino jijini Dodoma ambazo tayari zimeshauzwa


Mradi wa Iyumba Nyumba 1000

Mradi huu umejengwa eneo la Iyumbu (303) na Chamwino(101) Jijini Dodoma, nyumba nyingine mpya 68 ujenzi unaendelea eneo la Iyumbu na umefikia asilimia 90  na ujenzi wa nyumba 521 za makazi na biashara zimejengwa katika maeneo ya Mtukula-Kagera; Medeli-Dodoma na Dar es Salaam.


Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo katika mradi wake wa Iyumbu  Nyumba 1000 zilizojengwa  jijini Dodoma ambazo zimeshauzwa.


Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)zilizojengwa kupitia mradi wa Iyumbu Nyumba 1000 katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma ambazo tayari zimeshauzwa

Ukamilishaji wa miradi mikubwa ya Kawe 711 na Morocco Square


Mradi wa Kawe 711 ukiwa katika hatua za kukamilika katika eneo la Kawe Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Shirika katika kipindi hiki cha Awamu ya Sita, lilipanga kukamilisha miradi mikubwa iliyokuwa imesimama tangu mwaka 2018. Baada ya kuingia madarakani, Mheshimiwa Rais Dkt Samia aliikwamua miradi hii kwa kuliruhusu Shirika la Nyumba la Taifa kukopa hela za kuikamilisha miradi hii.

Morocco Square

Katika kipindi cha miaka minne ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Shirika limefanikiwa kukamilisha mradi wa Morocco Square kwa asilimia 100. Shirika linaendelea kuuza na kupangisha ambapo maeneo ya maduka (Retail Mall) yamepangishwa kwa asilimia 100 na Ofisi asilimia 95 imepangishwa.


Majengo ya Moroco Square mkoani Dar es Salaam


Tangazo lililopo karibu na makutano ya barabara katika eneo la Morocco Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam likionesha jengo la NHC ambalo limekamilika kwa asilimia 100 na lipo tayari kwa matumizi.

 

Katika jengo lenye nyumba za makazi 100, tayari nyumba 85 zimeshauzwa na mauzo ya nyumba zilizobakia yanaendelea.

Aidha, upangishaji wa Hoteli yenye vyumba 81 umefanyika kwa asilimia 100 na hoteli hiyo imeanza kutoa huduma.

Mkandarasi Estim Construction Company Limited alirejea katika mradi Januari 2024  na ujenzi wa mradi wa nyumba 422 pamoja na sehemu za biashara unaendelea katika mradi wa Kawe 711. Mradi huu una thamani ya Sh. Bilioni 169  ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2026.

Miradi wa “Samia Housing Scheme”


Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika Mradi wa Samia Housing Scheme zilizopo Kawe Manispaaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam(Oicha na Goodluck Hongo)

Ili kuenzi kazi nzuri ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani, na ili akumbukwe katika Sekta ya Nyumba, Shirika lilibuni mradi wa nyumba 5000 wa Samia Housing Scheme. Mradi huu umeleta matumaini mapya kwa wananchi. Katika eneo la Kawe, Dar es Salaam, ujenzi wa nyumba 560 ulianza na umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika Februari 2025.

Mradi huu utawezesha ujenzi wa nyumba 5,000 katika maeneo mbalimbali nchini zenye gharama ya Sh. Bilioni 466


Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika Mradi wa Samia Scheme zilizopo Kawe Manispaaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam(Oicha na Goodluck Hongo)

Mauzo ya nyumba 560 eneo la Kawe  yamekamilika na NHC inajiandaa kuanza awamu ya pili ya mradi huu eneo la Kawe (560) na Medeli Dodoma (100).


Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika Mradi wa Samia Scheme zilizopo Kawe Manispaaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam(Oicha na Goodluck Hongo)

Kwa ujumla, miradi ya Kawe 711 na Morocco Square inaenda kuboresha mandhari ya miji na kukuza uchumi wa Tanzania.

Utekelezaji wa ujenzi wa majengo ya kimkakati ya shughuli za Ofisi na biashara

Kahama Mkoa wa Shinyanga -Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Januari 2025.

Masasi Plaza –mkoani  Mtwara – Ujenzi wa jengo la biashara katika mji wa Masasi upo asilimia 40.

Mtanda Lindi- Ujenzi wa jengo la biashara Mtanda Commercial Building mkoani Lindi umefikia asilimia 30.


Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Lindi Omari Makalamangi akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maendelea ya ujenzi wa Mradi wa Mtanda Commercial Building


Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa jengo la kisasa la kibiashara la Mtanda Complex linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Lindi

2H Commercial Building – Morogoro – Ujenzi wa jengo hili la biashara lililopo katikati ya Manispaa ya Morogoro umefikia asilimia 40.

Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Ujenzi

Katika kipindi hiki, Shirika ni msimamizi na mshauri Elekezi wa miradi kadhaa ifuatayo:-

  • Usimamizi wa ujenzi Soko la Kariakoo wenye thamani ya Sh.Bilioni 28 umekamilika na ujenzi umefikia wastani wa asilimia 97. Mradi huu ulitarajiwa kukamilika Januari 2025
  • ) Usanifu na Usimamizi wa Jengo la Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango eneo la Mtumba umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 85 na Mjenzi ni Kampuni ya Estim Construction;


Jengo la Wizara ya Fedha na Mipango lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma linalojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililo katika hatua za mwisho kukamilika.(Picha na Goodluck Hongo)

  1. Usimamizi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira katika mji wa Serkali Mtumba jijini Dodoma awamu ya pili ujenzi umefikia asilimia 88 na Mjenzi ni Suma JKT;
  2. Usanifu na ujenzi wa Jengo la Soko la Madini (Tanzanite) eneo la Mirerani Manyara – Usanifu umekamilika na ujenzi umefikia asilimia 86.

Utekelezaji wa Sera ya Ubia

Baada ya kuingia madarakani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alifungua milango ya uwekezaji nchini na akahimiza ushirikiano wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma ili kuharakisha ujenzi wa uchumi wa Tanzania.

Shirika la Nyumba la Taifa ili kuenda sambamba na maono ya Mheshimiwa Rais, liliiboresha sera yake ya ubia na ikazinduliwa na Waziri Mkuu Novemba 16, 2022. Mwaka 2024 ambapo Shirika liliidhinisha na kusaini mikataba ya miradi 21 ya ubia yenye thamani ya Sh. Bilioni 179.

Kwa sasa Miradi 18 iliyopata vibali vya ujenzi imeanza kutekelezwa na ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za ujenzi. Miradi mingine mitatu imeshapata vibali hivi karibuni na itaanza kutekelezwa.

Aidha, Shirika limeendelea kusimamia miradi ya ubia ya sasa na ya zamani iliyokuwa imesimama ambayo ipo maeneo mbalimbali nchini.

Miradi minne iliyokuwa imesimama imesharejeshwa kwenye Shirika ili ikamilishwe na Shirika lenyewe.

Lengo la Shirika ni kuhakikisha miradi yote ya ubia isiyokamilika inarejeshwa katika Shirika na mazungumzo na wabia wenye miradi hiyo yanaendelea.

Kadhalika, Shirika linaendelea na mchakato wa upembuzi na tathimini ya kina kwa waombaji wapya kwa miradi mingine kwenye maeneo kadhaa yanayohitaji kuendelezwa na sasa iko kwenye hatua ya kupata idhini kwa ajili ya kuendeleza  viwanja hivyo visivyopungua 80 kwa nchi nzima.

Kupitia Sera ya Ubia, NHC limefanikiwa kushirikiana na Sekta Binafsi kujenga majengo ya kisasa ya makazi na biashara na kupendezesha mandhari ya miji yetu.

Eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam pekee lililokuwa na wapangaji 172 ambao nyumba zao zimevunjwa na kuendelezwa, sasa zitapatikana nyumba zaidi ya 2100 za makazi na biashara. Haya ni mageuzi makubwa sana.

Utekelezaji wa Miradi ya Ukandarasi

Katika kipindi cha Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, NHC ilipewa miradi kadhaa ya kimkakati ya ukandarasi yenye thamani ya Sh.Bilioni 186 ambayo imekamilika au ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji eneo la Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Ujenzi wa majengo ya Ofisi nane za Wizara umefikia asilimia 90.


Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Dodoma Omary Chitawala akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) Jengo la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambalo analisimamia wanalojenga katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Desemba 12,2024.Picha na Goodluck Hongo


Jengo la Wizara ya Kilimo lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma linalojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililo katika hatua za mwisho kukamilika.(Picha na Goodluck Hongo)


Jengo la Wizara ya Madini lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma linalojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililo katika hatua za mwisho kukamilika.(Picha na Goodluck Hongo)

Miradi mingine iliyotekelezwa na NHC katika Awamu hii ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo umefikia asilimia 80 na ni mradi unaogharimu Sh.Bilioni 9.7

Aidha, NHC inajenga jengo la Tanzanite huko Mererani, Manyara ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 86, Ujenzi wa Hospitali za Kanda ya Kusini (Mitengo) mkoani Mtwara  na Hospitali ya Kanda ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Musoma, Mara ambayo imekamilka na ukamilishaji wa Jengo la Kitengo cha Moyo cha Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ambayo nayo imekamilika kwa asilimia 100.

      Jengo la Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara ambalo limejengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)(Picha na Goodluck Hongo)


Leave a Comment: