Posted By Bajeti: 2025-02-06 07:30:52 |
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 66
Serikali yaendelea
na tathmini ya magugu maji Ziwa Victoria
NA MWANDISHI
WETU,DODOMA
NAIBU Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema Serikali
inaendelea na tathmini ya uwepo wa magugu maji katika Ziwa Victoria ili kupatia
ufumbuzi changamoto hiyo.
Khamis
ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma
Januari 31, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini Constantine Kanyasu aliyetaka kujua kama
Serikali inafahamu ongezeko la magugu maji katika Ziwa Victoria ikiwemo athari za magugu hayo na mpango wa
kuyadhibiti.
Amesema Serikali imechukua jitihada za kudhibiti magugu
maji katika ziwa hilo ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa na kutekeleza
Mkakati na Mpango Kazi wa Taifa wa Kukabiliana na Viumbe Vamizi wa mwaka
2019-2029 ambao unatoa mwongozo wa namna ya kuzuia kuingia na kuenea kwa viumbe
vamizi na una mipango endelevu ya kushughulikia viumbe vamizi waliopo na wale
wanaoweza kuingia.
“Mheshimiwa Spika, tathmnini inaendelea na nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute
subira wakati tunaendelea kulishughulikia jambo hili kwani limeendelea kuathiri
vyanzo vingi vya maji nchini kwa mfano Ziwa Jipe nalo lina changamoto ya
kuzingirwa na magugu maji,” amesema Khamis.
Ameongeza
kuwa Serikali inawajengea uwezo wananchi wanaoishi karibu na ziwa kuhusu namna
ya kujitolea katika kazi za kutokomeza na kuenea kwa magugu maji kila
yanapojitokeza ikiwemo kung’oa, kukausha na kuchoma magugu maji na kuendelea
kufanya tafiti mbalimbali ili kudhibiti uharibifu mifumo ikolojia ya Ziwa Victoria.
Aidha,
magugu maji yanaleta athari kwa mazingira, uchumi na kijamii ikiwemo kupungua
kwa oksijeni kwenye maji ambayo huzuia mzunguko wa hewa na mwanga wa jua hali
inyosababisha vifo vya samaki na viumbe wengine wa majini, uharibifu wa mifumo ikolojia na bioanuai ya Ziwa Victoria na huathiri maeneo ya mazalia
ya Samaki, shughuli za uvuvi na usafirishaji.
Katika
hatua nyingine, Naibu Waziri Khamis amebainisha kuwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura ya 191 imeweka msisitizo kwa miradi
yote mikubwa ni lazima ifanyiwe tathmini ya awali ya athari za mazingira kabla
ya mradi kuanza ili kuepuka uharibifu wa mazingira.
Aidha ameongeza kuwa Sheria pia inahimiza wananchi
kuhamasishwa kushiriki katika uhifadhi wa mazingira kupitia elimu, sheria ndogo
za serikali za mitaa, na mipango ya hifadhi ya mazingira.
Katika hatua nyingine Waziri Khamis amejibu swali la Mbunge wa Bahi Kenneth Nollo aliyetaka kujua Serikali ina
mpango gani wa kuweka Sheria kali
kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.
Akifafanuwa kuhusu swali hilo Khamis,ameeleza kuwa Sheria hiyo imeweka
msisitizo wa udhibiti wa uharibifu wa mazingira kwa kukataza uchafuzi wa maji,
hewa, na udongo kupitia kemikali za viwandani, kilimo, na shughuli nyingine za
binadamu.
‘’Serikali kupitia Wizara ya Maji imetenga fedha Sh.Bilioni 1.08 kwa ajili ya ukarabati wa Bwawa la Kalemawe lililopo katika Wilaya Same mkoani Kilimanjaro.
Akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum Naghenjwa
Kaboyoka aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuondoa tope lililojaa
katika Bwawa la Kalemawe – Same,Khamis amesema ukarabati umepangwa kufanyika katika robo ya nne ya mwaka wa fedha
2024/2025.
Ametaja shughuli zinzotarajiwa
kufanyika ni pamja na kukamilisha kazi ya usanifu wa kina na kuandaa gharama
kwa ajili ya ukarabati wa bwawa hilo kwa kuondoa tope, kukarabati utoro wa
maji, kujenga msingi wa tuta na tuta la bwawa.