Posted By Bajeti: 2025-02-19 08:58:45 |
Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 47
NA MWANDISHI WETU,DODOMA
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO)limesema kutakuwa na maboresho katika Kituo cha Kupokea ,Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo mkoani Dar es Slaam kuanzia Februari 22 hadi 28,2025
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma ya TANESCO Makao Mkuu Februari 19,205 imeeleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa Shirika katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake kufuatia ongezeko la mahitaji ya matumizi ya umeme katika maneo ya Zanzibar na mikoa ya Da es Salaam na Pwani ambalo limepelekea kituo hicho kuzidiwa na hivyo kulazimu kufungwa kwa Mashineumba(Tranformer) mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300 ili kukidhi mahitaji ya umeme katika maeneo tajwa.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa wakati kazi hizo zitakapofanyika baadhi ya maeneo ya Zanzibar na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yataathirika kwa kukosa umeme kwa nyakati tofauti.
"Aidha katika kipindi hicho ambacho huduma ya umeme itakosekana kwa nyakati tofauti,Shirika pia litakuwa likifanya matengenezo mbalimbali ya miundombinu ya umeme kwenye maeneo tajwa ili kuiweka miundombinu yetu kwenye hali ya uimara hasa kwenye kipindi hiki tunachoelekea msimu wa mvua.
''Shirika linaomba radhi kwa usumbufu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme itakosekana kwenye baadhi ya maeneo na litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo mpaka kukamilika kwake"imeeleza taarifa hiyo