Wassira: Kipaumbele cha CCM ni nchi kuwa na amani

Jamii habari

Posted By Bajeti: 2025-02-20 08:43:45 |

Share: Facebook | Twitter | Whatsapp | Linkedin Visits: 11


Wassira: Kipaumbele cha CCM ni nchi kuwa na amani

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Stephen Wasira amesema kipaumbele cha Chama wakati wote ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani.

Mbali na hilo lakini pia ameihakikishia Marekani kuwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu, utakuwa huru na wa haki.

Wasira amesema hayo Februari 20, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, aliyemtembea ofisini kwake katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizopo Lumumba.

Makamu Mwenyekiti Wasira amemweleza Kaimu balozi huyo kwamba, Tanzania ni Taifa linaloendelea, hivyo amani ya nchi haiwezi kuwekwa rehani.

Katika mazungumzo yao, wawili hao walizungumzia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini baadaye mwaka huu, ambapo Wasira alimhakikishia Lentz kwamba utafanyika kwa uhuru na haki.

"Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kujiandaa kushiriki uchaguzi huo na kinatarajia kushinda kwa sababu kimetekeleza ahadi za maendeleo zilizopo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025"amesema Wassira

Katika mazungumzo hayo Kaimu Balozi Lentz alitaka kujua kwamba je, CCM ipo tayari kuzungumza na vyama vya upinzani?

Akijibu swali hilo Wasira amesema CCM ipo tayari na ndiyo msingi wa falsafa ya R4 ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wasira ameongeza kuwa, R4 zinasisitiza mazungumzo pale ambapo kuna kutofautiana kimisimamo baina ya vyama.


Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)Stephen Wasira, Akizungumza na  Balozi wa Cuba  nchini Tanzania Yordenis Despaigne aliyemtembea ofisi kwake katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam Februari  20,2025

Katika hatua nyingine,Wasira amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini,Yordenis Despaigne.

Makamu Mwenyekiti Wasira na Balozi Despaigne  walikubaliana kuendeleza urafiki na ushirikiano wa maendeleo katika nyanja mbalimbali ambao umedumu kwa muda mrefu tangu wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza chini Hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Fidel Casto wa Cuba.

Leave a Comment: